Wednesday, March 7, 2012

WAJIBU WA WAZAZI KWA VIJANA NA WATOTO

UJUMBE UNATOKA: Kumb la torati 6:6-7
Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
tAFAKARI:
Kila kunapokucha tunashuhudia mpasuko mkubwa wa maadili kwa watoto na vijana wetu, pamoja na baadhi ya watoto kuwa na akili za kuzaliwa, watoto wengi wameharibikiwa na akili. Wengi ukiwaona wana uwezo mzuri, ila akili zao zimeharibiwa na malezi. Kumbuka Mungu anasema “Kumcha Bwana ni chanzo cha Maarifa…” Mithali 1:7. Wazazi wengi tunawalaumu watoto kwa kutokuwa waadilifu, ni jambo la kawaida kusikia “Heri nisingezaa kuliko kuwa na watoto kama hawa”. Mambo yafuatayo yanachangia kuharibu akili ya watoto:

1.      Wazazi hawana Muda wa kuwafundisha watoto neno la Mungu ambalo ndilo chanzo cha Maarifa yote ya uadilifu na kuwa na Hekima katika jamii, kuna wasomi wengi lakini sio wa kutegemewa katika jamii “They are hopeless”. Wazazi wengi wanakazania elimu ya kawaida, hiyo ni sawa, lakini elimu bila Mungu ni hatari, na ndicho tunachokiona siku hizi.

2.      Ugonvi  wa Wazazi na Maisha yasiyo na Amani na Upendo kati ya wazazi – Watoto wanaathirika kisaikolojia wanapoona Baba na Mama wanagombana, hasa wanapoona mmoja anaonewa, na mwingine kuonekana katili.  Watoto wako “very sensitive” na jambo hilo, na wakati wote wanakuwa ni “Upset Minded”, hali hii inaathiri uwezo wao wa akili. Wazazi acheni magonvi mbele ya watoto ni hatari.

3.      Malezi ya Mtoto yanaanzia Tumboni, hakikisheni mama akiwa mja mzito, ale vyakula vyenye virutubisho kwa ajili ya kujenga Afya na Akili ya Mtoto.  Hasira na Moyo wa huzuni kila mara huathiri mtoto tumboni. Vileo havitakiwi kabisa, vina athari kubwa kwa mtoto.

4.      Kumbuka chochote unachonena na kutenda mbele ya mtoto ndiyo elimu unayomfundisha. Kuna watu midomo haina Breki, wanaporomosha matusi hadi ya nguoni, ni wakali, na kila saa midomo iko juu, na tabia ya kuwadanganya watoto kuwa huyu ni Uncle, na usiku anahamia chumba cha baba na Mama, huo ni Uasherati na uzinifu, watoto lazima wataiga tabia hizo, na wakiwa vija wakubwa unaanza kuwalaumu.

5.      Chumba cha kulala kiwe na faragha, wazazi wengi wanalala na watoto, na vitoto vya siku hizi vinakomaa kabla ya wakati, utafikiri kamelala kumbe kanajisikilizia, huku kamefumba macho kabla hakajaiba kuchungulia. Hivi unafikiri michezo ya watoto ya Baba na mama unafikiri wanaitoa wapi?  wanaigiza hata mama anavyolia, kilio cha furaha. Kwa ujumla hayo ndiyo yanajaza akili zao hadi wanaenda kuchora kwenye karatasi za mitihani.

Wazazi wasilale na watoto chumba kimoja, pia chumba kiwe na milango inayofaa na dari lisiwe wazi, liwe na “sealing board”. Siku hizi nyumba za kupanga zimekuwa changamoto kubwa kuharibu tabia za watoto na vijana. Vyumba havina siri, Vijana na watoto hawapati usingizi usiku kwa sababu ya starehe kutoka vyumba visivyo na faragha. Wazazi watawajibika kwa kuharibu akili za Vijana na watoto wasipozingatia ushauri huu.

MUNGU AWABARIKI NA KUWAPATIA HEKIMA NA UWEZO WA KULEA WATOTO – NAWATAKIA SIKU NJEMA.

Ev:  Eliezer Mwangosi.
0755808077 & 0652571733
Kwa masomo zaidi fungua mitandao ifuatayo: http://emwangosi.blogspot.com/ (Vijana) http://kayanafamilia.blogspot.com/ (Ndoa) http://matengenezo.blogspot.com/ (Ujumbe wa Matengenezo)