Ujumbe unatoka: Mathayo 5:27-28
Mmesikia
kwamba imenenwa, USIZINI; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke
kwa kutamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
tAFAKARI:
Wiki
mbili zilizopita, Familia mbili ziliingia kwenye misiba ya kusikitisha baada ya
Baba wa familia moja na Mama wa familia nyingine kupata ajali ya gari na kufa
papohapo wakiwa wanatoka kupeana mapenzi. Mama (marehemu) alikuja likizo, mume
na watoto aliwaacha ulaya, na Baba (Marehemu) alikuwa anaishi hapa Dar na
familia yake, siku hiyo marehemu hawa walikutana, na wakakubaliana kukumbushia
mapenzi waliyokuwa wakipeana wakiwa marafiki kabla ya Ndoa. Shetani hakuwaachia
Pumzi, siku hiyohiyo ikawa ya RAHA na mara kugeuka kuwa ya HUZUNI NA MAUTI,
“One mistake one Goal”.
Marafiki
zangu, kama kuna adui mkubwa anayetesa familia katika vizazi vyote ni Dhambi ya
UZINZI, yaani Tendo la Ndoa kati ya watu wawili
wasio katika NDOA Halali. Familia nyingi zimesambaratishwa,
watoto wanahangaika utafikiri baba kafariki kumbe amesombwa na Kahaba, Familia
hazina Furaha wala Amani, Upendo umehamia kwa wenye kunyanyua Chuchu na Makalio
ya Mchina. Familia zinapata shida za pesa, huku akina baba wanaitwa mapedeshee,
mala ATM, Mabuzi na kila aina ya sifa, bila kusahau Mashugamamiii wanaojituliza
kwa vijana.
Kwa
bahati mbaya sana, Kila kunapokucha ndivyo Adui huyu mkubwa “ZINAA” anazidi
kupata umaarufu katika Jamii, anashabikiwa na kila Mtu, kuanzia watoto hadi
vikongwe, maskini hadi wafalme, wapagani hadi kwa manabii na Mitume feki. Ni
mara ngapi tumesikia vituko vya kwenye Ma “Guest House” vizito kuibiwa na
Machangu Doa, Makanisani wachungaji kula kondoo wao, mashuleni walimu na
wanafunzi, na vyuoni ndiyo usiseme, maofisini mabosi na wafanyakazi wao, na
zaidi hata kwenye mabasi (daladala) wanavyobanana, unashangaa mwanaume tayariiii
(Eti Mfadhaiko). HILO NI PEPO LA NGONO.
Amri
ya Saba katika zile Amri kumi inasema “USIZINI” Kutoka 20:14,
pamoja na kuhalalishwa na watu wengi, Mungu anasema “Ikimbieni
ZINAA. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye
ZINAA hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa MWILI wenu
ni hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi
si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu
katika miili yenu” 1Korintho 6:18-20. Kizazi cha NUHU na Sodoma Mungu aliwaangamiza
kwa sababu ya huyu adui Mtesaji na Muuaji “ZINAA”.
Wapendwa
tendo la Zinaa ni sawa na Kulamba Sukari iliyotiwa SUMU, na wengi hawajui hilo,
hatimaye wanaishia kwenye maisha ya Majuto na Kukata tamaa kama sio kifo, na
hatimaye Jehanamu ya Moto. Wengi wanadai huwezi kuishinda Zinaa, ni kweli, hata
Yesu alisema “Mimi ni Mzabibu; ninyi ni matawi;
akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; MAANA PASIPO MIMI NINYI
HAMWEZI KUFANYA NENO LO LOTE” Yohana 15:5. Ushindi wa dhambi hii ya
Zinaa, ni kwa, kuruhusu Roho Mtakatifu akaye ndani yetu, ambaye anaua
chembechembe za Virusi vya Dhambi (Tamaa ya mwili) na Kutupatia tabia ya Mungu
ndani ya MIOYO YETU, na huku ndiko kuzaliwa
UPYA.
SWALI
limeulizwa; je na wewe imepitiwa na huyu adui anayetesa familia? Jibu kwa
asilimia kubwa ni Ndiyo, hata kama wewe hujawahi kuanguka kwenye Zinaa, kwa
namna moja au nyingine umeyaonja madhara yake, kupitia familia tunazoishi nazo.
Wito wangu ni huu, wote walioathirika na jambo hili, Mlango bado uko wazi,
Rehema za Mungu bado zipo kutusaidia Kushinda na Kutuvusha salama.
BARAKA
ZA BWANA ZAKAAMBATANE NANYI WOTE DAIMA – NAWATAKIA SIKU NJEMA
Ev: Eliezer Mwangosi.
No comments:
Post a Comment